• Proceed to the Next Steps
    karibu

    IDARA YA WATOTO

    “Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.”

Kuhusu Sisi

Idara ya Watoto na Wanafunzi ni Idara ndani ya kanisa la TAG, lilianzishwa rasmi Mwaka 1994 kufuatia mkutano wa viongozi wa Kanisa la Assemblies of God, barani Afrika, “Africa Assemblies of God Alliance” (AAGA) uliofanyika Nairobi, nchini Kenya mwaka mwaka 1993. Idara hii ilianzishwa ikiwa ni utekelezaji wa maazimio muhimu katika mkutano huo wa (AAGA). Mwaka huo wa 1994 kanisa la TAG lilikuwa linaongozwa na Askofu Mkuu Rev. Ranwell Mwenisongole na alimteua marehemu Mchungaji Joseph Justine kuwa Mkurugenzi Mkuu. Kadhalika, marehemu Mchungaji Jeremiah Kimaro aliteuliwa kuwa Makamu Mkurugenzi Mkuu na Mch. Everhard Mloka kuwa Katibu Mkuu. Huo ndio ukawa mwanzo mzuri wa Idara hii.

Maono

Kuwafanya watoto wa Tanzania kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo, waliojazwa Roho Mtakatifu na kuukulia Wokovu, hatimaye wawe watumishi bora wa Bwana Yesu Kristo katika Kanisa lake.

Dhima

Idara ya watoto ipo ili Kumhubiri Kristokwa watoto wa Tanzania, mashuleni, mitaani, majumbani, Kanisani na kuwafanya wanafunzi wa Yesu Kristo.

Maadili ya Msingi

  • Ubora
  • Uaminifu kwa Biblia
  • Uadilifu
  • Wajibu kwa jamii
  • Kuwezesha viongozi